Back to top

Wadau wa usafirishaji watishia kugoma nchini.

23 May 2018
Share

Wadau wa sekta ya usarishaji abiria kwa kushirikiana na chama cha Madereva wa  Mabasi nchini wamejipanga kusitisha huduma ya usafiri nchini nzima ili kushinikiza SUMATRA kutekekeza agizo la Waziri Mkuu la kuwataka kukaa pamoja na wadau ili kufanya mapitio ya sheria na kanuni hizo mpya kama njia kutafuta ufumbuzi wa vipengele vinavyobishaniwa.

Wakizungumza katika stendi kuu ya Mabasi Ubungo,mwenyekiti wa chama cha Madareva wa Mabasi Bwana Shabani Mdemu ameitaka SUMATRA kusitisha kutoza faini kubwa zilizopo kwenye sheria na kanunu mpya zinazobishaniwa na kutekeleza agizo la Waziri Mkuu lililotaka wakae pamoja kufanya mapitio ya shirikishi ya kanuni na sheria hizo mpya.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TABOA Bwana. Enea Mrutu amewataka madereva hao kusitisha mpango wa kutaka kufanya mgomo kutokana na TABOA iko katika mchakato wa kuonana na viongozi wa juu wa serikali ili kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zilizomo katika sekta ya usafiri ikiwemo faini kubwa zinazotumika katika sheria na kanuni mpya ambazo tayari waziri mkuu ameagiza zifanyiwe kazi kwa kuwakutanisha wadau wote.

ITV imezungumza na kitengo cha mawasiliano cha wakala wa serikali wa uthibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini-SUMATRA- kuhusu malalamiko hayo, ambapo wamesema swala la utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu liko katika ngazi za juu,ikiwemo ngazi ya wizara uchukuzi.