Serikali shirika la hifadhi za taifa na wadau wa uhifadhi wameanza kuchukua hatua za kunusuru Ikolojia ya hifadhi ya ziwa Manyara na Tarangire kwa kuimalisha maeneo ya mapito ya wanyamapori (SHOROBA) yanayoathiriwa na shughuli za kibinadamu zinazotisha kukauka kwa ziwa Manyara na kutishia kufunga mapito ya wanyamapori (SHOROBA) wanaokwenda na kurudi katika hifadhi za Manyara na Tarangire
Wakuu wa wilaya ya Karatu Therecia Mahongo anasema mpango huo unahusisha kuwaondoa watu wanaofanya shughuli za kilimo holela katika maeneo hayo na wanaoharibu mazingira kwenye mapito ya wanyamapori.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya taifa ya ziwa Manyara Noelia Myonga anasema shughuli za kibindamu zinazofanywa katika maeneo ya miinuka katika wilaya za Karatu na Babati kwa kiasi kikubwa zimeathiri ziwa Manyara ambalo ndiyo tegemeo pekee la hifadhi hiyo.
Viongozi wa vijiji vinavyozunguka hifadhi pamoja na maeneo ya mapito ya wanyamapori wanasema wameanza kushirikiana na uongozi wa hifadhi katika kukomesha tabia hizo.