Back to top

Wadau waunga mkono mapambano ya Corona,kwa kutoa misaaada mbalimbali. 

28 March 2020
Share

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amepokea msaada wa fedha pamoja na vitu mbali mbali kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya corona (COVID-19) wenye thamani ya sh. bilioni 1.185 kutoka kwa wadau.

 
Amepokea msaada huo leo katika ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyoko Magogoni, Jijini Dar Es Salaam.

 Waziri Mkuu amewashukuru wadau hao na kuwataka Watanzania waendelee kushirikiana na Serikali katika hatua zinazochukuliwa kukabiliana na ugonjwa huo.

 
Miongoni mwa wadau waliotoa msaada huo ni taasisi za kifedha ikiwemo benki ya UBA Tanzania  iliyotoa sh. milioni 230, CRDB sh milioni 150 na  NMB sh milioni 100,wadau wengine ni  Karimjee Jivanjee Ltd,kampuni za gesi,shirikisho la wenye viwanda (CTI),Watoa Huduma ya Mafuta na Gesi Tanzania (ATOGS),Kampuni ya GS1 Tanzania Limited,Tanzania Oxygen ltd nakadhalika.
 
Kuhusu wadau wengine wanaohitaji kutoa misaada, Waziri Mkuu amesema Ofisi yake iko wazi pia wanaweza kupeleka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na kwa wanalio nje ya nchi au sehemu yoyote wanaweza kutuma fedha kupitia akaunti  yenye Jina la: National Relief Fund Electronic  Akaunti Na: 9921159801.