Jeshi la polisi limetumia mabomu ya machozi kuwatawanya waendesha boda boda na bajaji wanaofanya shughuli zao Posta mpya karibu na jengo la Benjamin Mkapa Tower baada ya uongozi kuwataka kuondoka katika maeneo hayo kwa madai kuwa hawaruhusiwi huku waendesha bodaboda na bajaji wakipinga hatua hiyo.