Waendesha pikipiki wilayani Arumeru mkoani Arusha wamelalamikia kuibuka kwa mtandao wa watu wanaokodisha pikipiki zao na baadaye kuwateka, kupora na kuwaua jambo linalosababisha washindwe kufanya kazi kwa amani hasa nyakati za usiku na wameomba serikali kufuatilia na kukomesha mtandao huo.
Vilio vya vijana wanaoendesha pikipiki vya kutekwa,kuporwa pikipiki na kisha kuuawa nyakati za usiku vimekuwa vikisikika katika maeneo mbalimbali nchini na licha ya kuwepo kwa jitihada kubwa za kuvikabili tatizo bado ni kubwa