Back to top

Wafanyabiashara katika kituo kikuu cha mabasi Moshi wamegoma.

15 February 2019
Share

Wafanyabiashara wa maduka zaidi ya 150 katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi mkoani Kilimanjaro wamegoma kufungua maduka wakipinga agizo la halmashauri ya manispaa ya Moshi ya kuwataka kulipa kodi  ya shilingi laki nne  hadi laki nne nusu  kwa kila pango kutoka  shilingi elfu 30 walizokuwa wanalipa awali. 

Wafanyabiashara hao wamemuomba Rais Dk John Pombe Magufuli kuingilia kati kutokana na baadhi ya wafanyabishara kushindwa kuendelea na biashara na kulazimika kurudi nyumbani. 

Wamesema ongezeko hilo ni kubwa sana hali ambayo inawakatisha tamaa kuendelea na biashara na kwamba fedha wanazozipata zinaishia kulipa kodi jambo hali  inayowarudisha nyuma kiuchumi.


Akijibu malalamiko hayo Mkurugenzi wa halamashauri ya manispaa ya Moshi Bw.Michael Mwandezi amesema uamuzi wa kupandisha kodi hizo ulipitishwa na vikao vya baraza la madiwani.