Back to top

Wafanyabiashara Msamvu walalamikia kuondolewa katika eneo la biashara.

11 November 2018
Share

Wafanyabiashara ndogondogo katika eneo la kituo kikuu cha mabasi cha Msamvu katika Manispaa ya Morogoro wamelalamikia kufukuzwa katika eneo wanapofanyia biashara zao kwasasa badala yake wahamie kwenye eneo jingine lisilo rafiki kwa biashara ili kupisha upandaji wa maua.

Hata hivyo Meneja wa Msamvu Property Company Limited wenye dhamana ya kusimamia kituo hicho kwa ubia na halmashauri ya Manispaa ya morogoro, amesema uamuzi huo umezingatia usalama wa abiria na kwamba hata kituo cha daladala ndani ya stendi kuu nacho kitahamishiwa upande wanakopelekwa wafanyabiashara hao hivyo  mzunguko wa mauzo yao utabaki palepale.