Back to top

Wafanyabiashara Mtwara waomba Meli kupeleka Vyakula Comoro.

14 April 2021
Share

Kufuatia kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan kwa waumini wa dini ya kiislamu baadhi ya wafanyabishara kwenye soko kuu mtwara wameiomba serikali kuwatafutia  meli ya kusafirisha vyakula kwenda kuuza nchini Comoro kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.
.
Wafanyabishara hao wa soko kuu Mtwara wamesema pamoja na kuwa na aina mbalimbali ya futari kwenye soko kuu hilo, kumekuwa na changamoto kubwa ya uhaba wa wateja unaotokana na ukosefu wa fedha. 
.
Aidha akizungumzia kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan Shekhe wa mkoa wa Mtwara Nurdin Mangochi amewataka waislamu kufuata maamrisho ya mwenyezi mungu ili waweze kupata thawabu huku Mkuu wa Wilaya wa Mtwara Bw.Dastan Kyobya akisema serikali imejipanga kuhakikisha huduma muhimu kama maji na umeme unapatikana wakati wote.