Back to top

Wafanyabiashara wa madini wanaotorosha madini ili kukwepa kodi waonywa

20 January 2019
Share

Serikali mkoani Ruvuma imewaonya wafanyabiashara  wa madini na kampuni za madini wanaotorosha madini kwa lengo la kukwepa kulipa kodi na tozo mbalimbali za serikali kwamba mkono wa sheria  hautawaacha salama.

Onyo hilo limetolewa na  mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Pololeti Kamando Mgema kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma wakati akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa madini ulioshirikisha wachimbaji wadogo wa madini na makampuni makubwa ya madini mkoani Ruvuma na viongozi wa serikali.

Afisa madini wa mkoa wa Ruvuma Bw.Abraham Nkya anasema kuwa kwa kushirikiana na vyama vya wachimbaji wa madini katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha wa 2018/2019 wamekusanya kodi na tozo mbalimbali kiasi cha shilingi bilioni 2 na milioni 700 kati ya shilingi bilioni 2 na milioni 800 walizopangiwa.