Back to top

Wafanyabiashara waendelea kulia na uhaba wa mafuta ya kupikia nchini.

23 January 2021
Share

Wafanyabiashara wa jumla wa mafuta ya kupikia katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam wamesema licha ya serikali kudai shehena ya mafuta kutoka nje ya nchi imewasili na kuanza kusambazwa bado bei ya mafuta inaendelea kupanda na mafuta hata viwanda vya ndani hakuna na kusababisha wananchi kuendelea kupata shida.

ITV imepita katika maduka mbalimbali yanayouza mafuta ya kupikia kwa bei ya jumla na wafanyabishara hao kudai bei bado iko juu licha ya kusikia uwepo wa shehena ya mafuta kuwasili nchini lakini bei ya mafuta kwa wiki moja iliyopita dumu la lita ishirini limepanda kutoka elfu sabini mpaka elfu 84 na na mafuta hayo kwa viwanda vya ndani hayapatikani pia.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wanaouza vitafunwa chipsi na vyakula katika maeneo mbalimbali ya jiji wamesema kutokana na mafuta kuendelea kupanda bei kwa sasa inabidi wapungunze vipimo vya chipsi huku wauza maandazi na chapati wakipandisha bei.

Hivi karibuni serikali kupitia wizara ya viwanda na bishara imenukuliwa na vyombo vya habari ikikiri kuwepo kwa uhaba wa mafuta na kwamba utamalizika siku chache zijazo baada ya kuwasili kwa meli za mafuta nchini.