Back to top

Wafanyabiashara walia na gharama za chumvi Mtwara.

23 July 2018
Share

Wafanyabiashara wa Chumvi katika Mkoa wa Mtwara wamesema licha ya serikali kutoa madini joto bure yanayochanganywa kwenye chumvi wako baadhi ya watu wamekuwa wakiwauzia bidhaa hiyo kwa bei ya Shilingi Elfu Sabini kwa kilo na hivyo kufanya baadhi ya watengenezaji chumvi kushindwa kumudu gharama na kujikuta chumvi nyingi inaingia sokoni bila kuwa na madini joto.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Watengeneza Chumvi Mkoa wa Mtwara, Bwana  FESTO BALEGELE ambaye amesema kukosekana madinijoto katika chumvi kunaathari kubwa hasa kwa watoto wadogo.