Back to top

Wafanyakazi 379 wa ujenzi barabara ya Mpemba-Isongole wagoma.

14 December 2018
Share

Wafanyakazi 379 wanaotekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya lami ya  Mpemba - Isongole  mkoani Songwe wamegoma kuendelea na kazi kwa muda usijulikana wakishinikiza mkandarasi wa kampuni ya China Geo Engeneering corporation kuwalipa madai yao ya fedha ambazo hawajalipwa takribani miezi 17 hadi sasa.

Mgomo huo wa wafanyakazi unashinikiza uongozi wa kampuni kulipa deni la malimbikizo ya miezi 17 kwa siku za jumamosi na jumapili na kupandisha malipo ya fedha kwa gharama ya chakula kutoka sh. 500 waliyokuwa wakilipwa awali hadi 2500 kwa siku.

Madai mengine ni uonevu unaofanywa na wachina dhidi ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kutojali malalamiko yao, na upande wa serikali kukosa usimamizi mzuri wa haki za wafanyakazi ikiwemo upatikanaji wa vifaa kinga vya kazi na namna vinavyotumika.

Kufuatia mgomo huo viongozi wa wakala wa barabara mkoa wa Songwe na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ileje umepata wakati mgumu kushawishi pande mbili kuweka makubaliano kutokana na  msimamo mkali wa wafanyakazi, hali iliyomlazimu mkandarasi kukubaliana na matakwa yao na kuahidi kutekeleza malipo yote ndani ya wiki moja.