Back to top

wafanyakazi watatu wa Mugabe wapandishwa kizimbani kwa tuhuma za wizi.

11 January 2019
Share

Wafanyakazi watatu wa rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe wamefikishwa mahakamani wakishtakiwa kuiba mkoba uliokuwa na dola za kimarekani 150,000  mali ya Mugabe.

Washtakiwa hao wanadaiwa kutumia pesa hizo kununua magari, nyumba na mifugo.