Back to top

Wafuasi 9 wa Khamenei wawekewa vikwazo na Marekani.

05 November 2019
Share

Marekani imesema inaweka vikwazo kwa raia tisa waliopo karibu na Kiongozi Mkuu wa Iran ambao wanaukaribu na kiongozi mkuu wa nchi hiyo Ali Khamenei.

Wizara ya Fedha ya Marekani imesema watu tisa ni pamoja na mkuu wa mahakama ya Iran na mtoto wa pili wa kiume wa kiongozi mkuu wa Iran.

Watu hao mali zao zilizopo nchini Marekani zitazuiwa pamoja na hatua zingine, Khamenei mwenyewe aliwekwa kwenye orodha ya watu waliopigwa marufuku mnamo mwezi Juni.

Waziri wa Fedha wa Marekani Steven Mnuchin amesema katika taarifa yake kwamba watu hao tisa wanahusika na mambo mabaya kadhaa ya utawala wa Iran.

Mapema Ikulu ya Marekani iliwaonya katika taarifa juu ya vikwazo zaidi vya udhoofishaji hadi Iran ibadili mwenendo wake wa uhasama.