Back to top

Wafugaji Mbarali wagoma kumega ardhi yao kuwapa wakulima.

31 October 2018
Share

Wafugaji  wa jamii ya kimasai ambao wameachana na ufugaji wa kuhama hama unaoharibu mazingira  wilayani Mbarali mkoani Mbeya wamesema hawako tayari kuona ardhi yao ikimegwa na serikali ya wilaya ili kuwapa wakulima.

Wametoa msimamo huo mbele ya mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mbarali, Ibrahim Mwandungu ambaye amefika katika kijiji cha Matebete kwa nia ya kusikiliza kero za wananchi hao.