Back to top

Wafugaji wawacharaza viboko walinzi wa hifadhi ya msitu, Tanga.

16 April 2021
Share

Wakina mama pamoja na baadhi ya viongozi wa kijiji cha Mkonde kilichopo wilayani Kilindi mkoani Tanga wanaolinda msitu wa hifadhi ya Mbwego wamechapwa viboko na wafugaji wakati wakijaribu kukamata mifugo ilioingizwa kwenye hifadhi hiyo kinyume na utaratibu.
.
ITV imefika kwenye msitu huo wenye zaidi ya hekta elfu moja na mia tano na kushuhudia mzozo huo baina ya wafugaji  pamoja na viongozi hao.
.
Hata hivyo katika hali ya kushangaza wakati wanachi hao wakishiriki kupanda miti iliotolewa na wadau wa kuongeza thamani ya mazao ya misitu FORVAC mwenyekiti wa kijiji hicho aliamuru mifugo hiyo iachiwe jambo lililopingwa na kamati ya ulinzi wa msitu huo.
.
Vurugu hizo zilisababisha kusimama kwa muda zoezi la upandaji miti kwenye mpaka wa msitu huo hali iliyosababisha mwakilishi wa FORVAC kuelezea dhamira yao huku kaimu afisa misitu akielezea athari zinazoweza kutokea kwenye msitu huo kutokana na  wafugaji kuingiza mifugo kwenye hifadhi hiyo.