Back to top

Wafungwa 259 gereza la Ruanda Mbeya watoka kwa msamaha wa Rais JPM.

10 December 2019
Share

Wafungwa 259 Gereza la Ruanda mkoani Mbeya wametoka kufuatia msamaha wa Rais Dkt.John Magufuli alioutoa Disemba 9, 2019 wakati wa Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri zilizofanyika CCM Kirumba Mwanza.

Baadhi ya wafungwa walionufaika na msamaha huo, wamemshukuru Rais, Dk.John Magufuli kwa kuwasamehe na kuahidi kwenda kuishi kwa uadilifu na kufanya Kazi za Maendeleo. 

Ndugu na jamaa wa wafungwa walioachiwa huru nao wamemshuru Rais Magufuli wakidai kuwa ndugu zao wamekaa muda mrefu gerezani na hawakuwa na matumaini ya kuwaona ndugu zao wakiwa huru, lakini Rais Magufuli amefanya jambo hilo kuwezekana.
 
Wakati wa Sherehe za Miaka 58 ya Uhuru na 57 ya Jamhuri Rais Magufuli zilizofanyika Disemba 9, 2019 CCM Kirumba Mwanza aliainisha wafungwa ambao amewapa msamaha akisema unawalenga zaidi wafungwa waliofungwa Kati ya siku moja na mwaka mmoja.

Aliongeza Rais Magufuli kuwa Wafungwa wengine watakao husika na msamaha huo ni wafungwa waliofungwa miaka 30, miaka 20, miaka 10, miaka 5, lakini tayari wametumikia sehemu yao kubwa ya vifungo vyao na kubakiza kipindi kisichozidi mwaka mmoja watahusika na msamaha huo.