Back to top

Wagonjwa wa Corona Kenya wafikia 465.

03 May 2020
Share

Wizara ya afya nchini Kenya imethibitisha maambukizi mapya 30  ya virusi vya corona hii ni baada ya sampuli 883 kufanyiwa vipimo katika muda wa saa 24 na kufanya idadi ya walioambukizwa kufikia  465 .

Naibu waziri wa afya Dk Rashid Aman anasema kuwa  19 ni wagonjwa kutoka Mombasa, 8 jijini Nairobi wawili kaunti ya Bungoma na kimoja kaunti ya Kitui.

Watu wawili zaidi aidha wamefariki kaunti ya Mombasa  kutokana na virusi hivyo na kufikisha waliofariki nchini Kenya kuwa 24 na idha waliopona ni  167 baada ya watu 15 zaidi kuruhusiwa kuondoka hospitalini.

Wizara ya afya ikihofia kutokana na idadi ndogo ya watu wanaojitokeza kupimwa kwa hiari baada ya vipimo vya halaiki kuanza katika mitaa ya Estleigh na  Kawangware hapa jijini Nairobi.