Back to top

Wagonjwa wawili wapandikizwa figo na madaktari wazawa Dodoma.

02 July 2020
Share

Katika kupunguza gharama zaa kusafirisha wagonjwa wa figo kwenda kutibiwa nje ya nchi hatimaye hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo Makao Makuu ya nchi Dodoma  imefanya matibabu ya kupandikiza figo kwa wagonjwa wawili kwa kutumia madaktari wazawa bila kutumia madaktari kutoka nje ya nchi na kufikisha jumla ya wagonjwa 13 waliopandikizwa figo katika hospitali hiyo.

Akitoa taarifa mara  baada ya kufanya upandikazaji huo kwa mtu wa pili, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Dk Alphonce Chandika amesema lengo la hospitali hiyo ni kuwa hospitali bingwa ya kutibu figo nchini.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya figo hospitalini hapo, Dk Kessy Shija amesema kitendo cha serikali kuwekeza vifa tiba kwenye hospitali hiyo kumefanikisha watanzania wengi kupata matibabu ndani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha corona ambapo mipaka ya nchi nyingi ilifungwa.