Back to top

Wahadzabe,Watatoga na Wairaq wanogesha tamasha la URITHI wa Utamaduni

19 October 2019
Share

Wananchi wa jamii za wafugaji, wawindaji na waokota matunda wamekuwa kivutio kikubwa katika tamasha la URITHI wa Utamaduni wa asili linalofanyika kitaifa katika wilaya ya Karatu mkoani Arusha .

Wakizungumza wakati wa tamasha hilo viongozi wa baadhi jamii hizo ikiwemo ya Wahadzabe, Watatoga,na Wairaq pamoja na kuonesha utamaduni wao ukiwemo wa Ngoma, vyakula, dawa na zana za asili wameiomba serikali kuyàlinda maeneo yao ya asili na kuhakikisha yanatambulika kama ya urithi wa Watanzania .

Mratibu wa maonesho hayo Bw.Agnery Chitukuro amesema mwitikio mkubwa wa wananchi wa jamii hizo katika tamasha hilo ni dalili njema za kuonyesha kuanza kutambua thamani ya utamaduni wa asili.

Mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha la URITH wa Wtamaduni nchini Bw.Martin Muhando amesema tamasha hilo pamoja na kuanza kuvutia wananchi na pia wageni kutoka nje, linadhihirisha namna Tanzania ilivyo na utajiri mkubwa wa tamadumi za asili ambazo licha ya kuwa na thamani kubwa bado hazijaweza kusaidia kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Tamasha hilo  la siku tatu linatarajiwa kufungwa na Waziri wa Habari Dr.Harrison Mwakyembe.