Back to top

Wahamiaji haramu 50 wakamatwa Bagamoyo,wapelekwa kituo cha afya.

19 March 2020
Share

Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Bagamoyo ikiongozwa na Mkuu wa wilaya hiyo Mh Zainabu Kawawa imekamata zaidi ya wahamiaji haramu 51 kutoka nchi za Ethiopia na Somalia wakiingia nchini kupitia mipaka ya wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa kutumia majahazi.

Akiongea baada ya kuwakamata wahamiaji hao Mkuu wa wilaya hiyo Mh. Zainabu Kawawa amewaonya wananchi wote wanaojiusisha katika kuingiza wahamiaji hao kuacha mara moja vitendo hivyo huku akisema watakaobainia kushirikiana nao watachukuliwa hatua za kisheria.

Aidha Mh Kawawa amesema kwa sasa wameimarisha ulinzi katika mipaka ya wilaya hiyo ambapo wahamiaji hao baada ya kukamatwa wamepelekwa katika kituo cha afya cha Matimbwa na kuanza kufanyiwa vipimo kutokana na uwepo wa ugonjwa wa virusi vya corona.