Back to top

Wahamiaji haramu wakamatwa mkoani Rukwa.

11 January 2019
Share

Idara ya uhamiaji mkoani Rukwa imewakamata wahamiaji haramu, wakiwa ni raia wa nchi za Ethiopia, Somalia na Zambia, katika msako mkali unaoendelea hivi sasa mkoani humo, wakiwa wanasafirishwa kwenda mji wa Tunduma mkoani Songwe.

Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Rukwa Naibu Kamishna wa uhamiaji Elezius Mushongi amesema pia wanawashikilia Watanzania wawili waliokuwa wakiwasindikiza wahamiaji hao wa Kihabeshi na Kisomali, ambao hivi sasa wamebuni mbinu mpya ya kusafiri wachache wachache kukwepa mitego.