Back to top

Wahamiaji washikiliwa kwa kukutwa na vitambulisho vya kupigia kura

09 February 2019
Share

Wahamiaji 100 kutoka nchi saba za kiafrika na moja ya kiarabu ambao ni walowezi walioishi nchini kihalali kwa muda mrefu na baadae muda wao kumalizika wamekamatwa na kutozwa faini ya shilingi milioni 14.7 na wengine wawili wanashikiliwa na idara ya uhamiaji mkoani Kilimanjaro kwa kughushi nyaraka za kuishi, uraia na kukutwa na vitambulisho vya wapiga kura.

Kamishna msaidizi wa uhamiaji wa mkoa huo kamanda Albert Rwelamira amesema, wahamiaji hao  wamekamatwa katika  wilaya za Same, Siha na Moshi  katika oparesheni maalum inayoendelea ambayo watu waliotozwa faini wametoka nchini za Zambia, Msumbiji, Malawi, Rwanda, Burundi,Kenya, Uganda,Omani na wengine wanachunguzwa.

Kamanda Rwelamira amesema, raia wawili Antony Okello wa Kenya na Richard Mutasa wa Uganda  ambao ni waalimu wa shule za Bendel na Mary Gorate wamekutwa wakiwa na nyaraka za kughushi zikiwemo za kuishi nchini, vyeti vya kuzaliwa pamoja na wazazi wao kwa majina tofauti  na vitambulisho vya wapiga kura ambavyo wamepiga kura navyo mara kadhaa.

Raia hao wa kigeni  wamekiri kughushi nyaraka hizo na wameiomba radhi serikali ya Tanzania kwa kitendo hicho ambacho wamedai  walikifanya  bila kujua  baada ya kudanganywa na watu wachache wenye dhamana ambao walikuwa na  uchu wa kujipatia fedha za haraka haraka kutoka kwao.