Back to top

Wahujumu wa miundombinu ya TANESCO waanza kusakwa.

16 June 2019
Share

Shirika la umeme nchini (TANESCO) limeanza operesheni kwa mikoa ya kanda ya ziwa ukiwemo mkoa wa Mwanza ya kuwabaini wadaiwa sugu wa shirika hilo pamoja na wale wote wanaohujumu miundombinu ya TANESCO kwa kuzichezea mita ili kukwepa kulipa ankara.

Akiongoza operesheni hiyo iliyoanzia eneo la Igogo jijini Mwanza na inayotarajiwa kufanyika nchi nzima lengo likiwa kuhakikisha umeme unaozalishwa unaendana na kiasi cha fedha kinachopatikana ili huduma hiyo iweze kuwa na tija pamoja na kudhibiti vitendo vinavyokwamisha utendaji wa shirika hilo.

TANESCO katika mikoa ya kanda ya ziwa ina zaidi ya wateja laki tatu, ambapo deni wanalodaiwa  baadhi ya wateja wa shirika hilo ni kiasi cha shilingi bilioni tisa, deni ambalo linatajwa kurudisha nyuma ufanisi wa shirika hilo kiuendeshaji.