Back to top

Wahukumiwa kwenda jela kwa wizi wa mtoto mchanga wa siku 7 Ruvuma.

15 June 2019
Share

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi.Christina Mndeme amemkabidhi kwa mama yake Amina Abdalah mtoto wa kike aliyeibwa akiwa na siku saba na sasa ana miezi tisa huku aliyeiba mtoto huyo Abraham Kilewa na aliyeuziwa  kwa shilingi elfu 30 Anusiata Luambano wakifungwa mwaka mmoja kila mmoja.


Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma ACP Simon Marwa anasema kuwa mtoto huyo aliibiwa Septemba 2018 na Abraham Kilewa ambaye alimuuza kwa mfanyabiashara anusiata luambano mkazi wa mkoani kilimanjaro kwa shilingi elfu 30.


Kwa upande wake Mganga mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt Jairy Khanga amesema kuwa kitendo kilichofanywa na watu hao ni cha ukatili kwani walimkosesha mtoto haki ya malezi toka kwa wazazi wake.


Akimkabidhi mtoto huyo kwa mama yake mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bi. Mndeme amempa zawadi ya shilingi laki tatu kwa askari polisi Victor Nkonya kwa kufanikisha kupatikana kwa mtoto huyo huku akitoa wito kwa wanaohitaji watoto kwenda vituo vya kulelea watoto yatima na si kutumia njia ya wizi.