Back to top

Wajasiliamali Kagera wahimizwa kusindika vyakula vyenye virutubisho.

20 April 2019
Share

Wajasiliamali katika mkoa wa Kagera wanaojihusisha na shughuli za usikindaji wa bidhaa aina mbalimbali za vyakula wametakiwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA) yanayowaagiza wasindike vyakula vyenye virutubisho vya kutosha ili waweze kuimarisha miili ya walaji jambo litakalosaidia kupunguza tatizo kubwa linaloukumba mkoa huo kwa sasa la utapiamulo na udumavu wa akili linalochangiwa na lishe duni.
 
Hayo yameelezwa na Mwakilishi wa mkurugenzi wa usalama wa chakula TFDA  Justine Ngaleimaki baada ya mganga mkuu wa mkoa wa Kagera Dkt. Marco Mbata kueleza hali ya kiwango cha utapiamulo na udumavu wa akili katika mkoa na mambo yanayochangia tatizo hilo.