Back to top

Wajasiriamali soko la Kiwira walalamika kutozwa ushuru.

23 July 2020
Share

Wafanyabiashara wadogo wa mboga na matunda katika soko la Lembuka lililopo Kiwira wilayani Rungwe, wamelalamika kuwa licha ya kununua vitambulisho vya wajasiriamali vilivyotolewa na rais, bado halmashauri ya wilaya ya Rungwe inaendelea kuwatoza kodi pamoja na kudai ushuru wa mazao yasiyozidi tani moja kinyume na  maelekezo ya rais Magufuli.

Wafanyabiashara hao wamesema hawaoni umuhimu wa vitambulisho vya ujasiriamali ambavyo vimetolewa na Rais kutokana na halmashauri ya wilaya ya Rungwe kuendelea kuwatoza ushuru kinyume na maelekezo waliyopewa kabla ya kununua vitambulisho hivyo.

Mwenyekiti wa soko hilo,Bw.Juma Asante amesema baada ya kupata malalamiko ya wafanyabiashara hao,alichukua hatua za kuiandikia barua halmashauri hiyo,lakini hakuna hatua zilizochukuliwa na badala yake wameendelea kuwanyanyasa wafanyabiashara hao.