Back to top

Wajawazito kijiji cha Nyakunguru Tarime wajifungulia njiani.

17 September 2019
Share

Naibu waziri ofisi ya rais, tawala za mikoa na serikali za mitaa ( TAMISEMI ) Mhe.Mwita Waitara ametoa muda wa miezi mitatu kwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Tarime mkoani Mara kukamilisha ujenzi wa zahanati ya Itandura katika kijiji cha Nyakunguru ili kumaliza changamoto ya baadhi ya wakinamama wajawazito kujifungulia njiani na wengine kupoteza maisha kutokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Mhe.Waitara ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wakazi wa kijiji cha Nyakunguru, baada ya kukagua jengo la zahanati ya Itandura ambalo halijawahi kutumika kwa kipindi cha miaka 39 tangu lililopojengwa, ambapo amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Apoo Tindwa pamoja na mkuu wa wilaya ya Tarime mhandisi CharlesKkabeho kutumia zaidi ya shilingi milioni 100 zilizotolewa na mgodi wa Acacia North Mara kumalizia ukarabati wa jengo hilo na kujenga nyumba ya mganga, choo na kichomea taka ifikapo disemba mwaka huu.

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha nyakunguru wanaeleza adha wanayoipata kutokana na kijiji hicho kutokuwa na zahanati kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, kaimu mganga mkuu wa wilaya ya tarime dk. Amidu adrian amesema hadi sasa zahanati hiyo ina jengo moja tu la wagonjwa wa nje, hali ambayo inatatiza utoaji wa huduma za afya kwa ufanisi.