Back to top

Wakamatwa wakijaribu kuuza dhahabu feki soko la madini Mbeya.

15 February 2020
Share

Watu wawili akiwemo mwalimu wa Shule ya Msingi Nkangamo wilayani Momba Mkoani Mbeya wanashikiliwa na polisi baada ya  kukutwa na kipande cha dhahabu bandia chenye uzito wa zaidi ya gramu 600 wakijaribu kukiuza katika soko kuu la madini wilayani Chunya.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la polisi, Ulrich Matei amesema tukio hilo limetokea February 14 kwenye soko kuu la dhahabu wilayani,na kwamba endapo  watuhumiwa wangefanikiwa kuuza kinde hichi cha dhahabu wangejipatia ya zaidi ya shilingi milioni 70 kinyume na sheria.