Back to top

Wakamatwa wakiuza mita za maji zisizokaguliwa Singida.

20 September 2020
Share

Wakala wa vipimo mkoa wa Singida umebaini baadhi ya maduka ya ujenzi mkoni humo wanauza mita za maji ambazo hazijakaguliwa na hazina sili,jambo ambalo limekuwa likisababisha watumiaji wa maji kulipa bili ndogo au kubwa kwasababu mita hizo hazija kaguliwa na Wakala wa Vipimo.
 
Baada ya ukaguzi katika baadhi ya maduka ya ujenzi Manispaa ya Singida Meneja wa Wakala wa Vipimo mkoa wa Singida Bwana Raurent Kabikiye amesema wamiliki hao watachukuliwa hatua za sheria ya vipimo.

Katika hatua nyingine Meneja wa Wakala wa Vipimo mkoa wa Singida amewataka wafanyabiashara kuepuka kuingia kwenye mkono wa sheria na kuathiri biashara zao.