Back to top

Wakandarasi wa umeme nchini watakiwa kukabidhi miradi ya umeme mapema

20 June 2020
Share

Bodi za REA na TANESCO zimewataka wakandarasi nchini kukamilisha ujenzi wa miradi ya umeme mwishoni mwa mwezi huu kama ilivyoagizwa na waziri wa nishati ambapo aliwataka wakandarasi watakaoshindwa kumaliza ujenzi watasitishiwa mikataba yao pamoja na kukatwa asilimia kumi ya malipo yao.

Akizungumza mara baada ya kutembelea miradi ya umeme mkoani Geita mkurugenzi wa bodi ya umeme vijijini REA Oswardi Urassa anasema wameanza kukagua ujenzi wa miradi ya umeme kwa mikoa yote ili kuhakikisha miradi yote inakamilika kabla ya kuanza miradi mingine.

Wakandarasi wanaojenga miradi ya umeme kwa mikoa ya kanda ya ziwa wanasema wanaendelea kufanya kazi usiku na mchana ili kumaliza miradi kwa wakati huku changamoto kubwa ilikuwa mafuriko na kuchelewa  kuingia kwa vifaa kutokana na maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Waziri wa nishati Dkt.Medard Kalemani ameziagiza bodi za REA na TANESCO kuwasimamia usiku na mchana wakandarasi ili waweze kumaliza miradi yote kwa wakati.