Zaidi ya wakazi elfu thelathini na sita wa kata ya Majimoto katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi watanufaika na huduma ya nishati ya umeme ikiwemo kuondokana na adha ya kutumia tochi katika zahanati baada ya mradi wa kusambaza nishati ya umeme vijijini (REA) awamu ya tatu kuanza kutekelezwa mkoani humo.
Akizungumza na wananchi wa kata ya Majimoto waziri wa nishati Dkt. Medard Kalemani amesema mradi huo kwa awamu hii utaunganisha umeme katika taasisi zote za umma ,vijiji vyote na vitongoji vyake
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mlele Bi.Rachel Kasanda amesema wilaya ina jumla ya viwanda 236 ambapo 30 kati ya hivyo ni viwanda vya kati huku asilimia 60 vikiwa katika kata ya majimoto
Mradi huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka miwili unatarajiwa kukamilika mwezi juni mwaka 2020.