Back to top

Wakazi makorora mkoani Tanga wakarabati barabara

20 July 2018
Share

Wakazi zaidi ya 400 wa mtaa wa makorora uliopo kata ya makorora jijini Tanga,wamejitolea kukarabati barabara chakavu inayounganisha eneo hilo kwenda kata ya mabawa kufuatia mvua zilizonyeesha hivi karibuni kuharibu vibaya daraja kuu linalopitisha maji kwenda baharini hatua inayosababisha nyakati za mvua wanafunzi kuwa watoro kwa kuhofia kusombwa na maji.

Wakizungumza katika eneo la mtaa huo wakati kazi za ukarabati zilizokuwa zikiongozwa na mbunge wa jimbo la tanga mheshimia mussa mbaruk zikiendelea,baadhi ya wananchi wa eneo hilo hilo ameelezea changamoto kubwa zinazosabsbishwa na kuvunjwa ka daraja hilo.

Kufuatia hatua hiyo mbunge wa jimbo la tanga mheshimiwa mussa mbaruk amewataka watendaji wa taasisis zinazojihusisha na ukarabati a miundo mbinu ya maji wanapomaliza kazi zao maeneo ya barabara ni vyema wakarudishia miundo mbinu kama ilivyo kuwa awali.