Back to top

Wakazi zaidi ya 1600 wakosa mawasiliano ya barabara kwa miezi 4.

10 November 2018
Share

Wakazi zaidi ya 1600 wa vijiji vitatu vinavyonganisha wilaya za Ileje na Mbozi mkoani Songwe hawana mawasiliano ya barabara kwa zaidi ya miezi minne kufuatia daraja la mto Hantesya linalounganisha wilaya hizo mbili kusombwa na maji ya mvua na hivyo kusababisha shughuli za kiuchumi za wakazi hao kusimama.

Wakizungumza katika eneo la daraja hilo lililosombwa na maji ya mvua viongozi wa serikali ngazi za kijiji pamoja na wakazi wa kijiji cha Hantesya, wamesema wanashindwa kusafirisha mazao yao ya biashara na chakula, wanafunzi kushindwa kwenda shule sanjari na kusafirisha wagonjwa kuwapeleka katika zahanati na vituo vya afya baada ya watu 10 kupoteza maisha miezi miwili iliyopita.

Katika kukabiliana na changamoto hiyo baadhi ya wakazi ambao walikuwa wamekata tamaa baada ya kukosa mawasiliano wameamua kujitolea nguvu kazi na kuiomba halmashauri ya wilaya ya Mbozi kusaidia zoezi hilo.

Kufuatia hatua hiyo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Mbozi kazi mbaya Makwega pamoja na timu ya watendaji waliofika kukagua daraja hilo amesema halmashauri kwa kushirikiana na mbunge wa jimbo hilo watalifanyia ukarabati daraja hilo ili shughuli za wananchi za uzalishaji mali ziweze kuendelea.