Back to top

Wakijiji Mara wakataa mradi kwa madai umejengwa chini ya kiwango.

21 August 2018
Share

Wananchi wa kijiji cha Kirogo wilayani Rorya wa mkoani Mara, wamekataa kuupokea mradi mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.1 ambao umejengwa na kampuni ya ujenzi ya M/S Contrive Engineering CO. Limeted ya mjini Musoma, baada ya kubaini kuwa mradi huo umejengwa chini ya kiwango.

Wakizungumza mbele ya Waziri wa maji na umwagiliaji Prof Makame Mbarawa, wananchi hao wakiongozwa na viongozi wa serikali katika maeneo hayo, wamesema kuwa tangu mkandarasi huyo adai tayari amekamilisha ujenzi wa mradi huo mwaka 2016,hadi sasa  mradi huo umeshindwa kutoa maji kwa ajili ya kuwafikia wananchi.

Nkwande Bulele, akizungumza katika eneo la tukio,ameonesha kusikitishwa na wananchi hao kudai mbele ya waziri kuukataa mradi huo,wakati wamesaini makabidhiano baada ya kuridhishwa kuwa mradi huo umejengwa kwa kiwango kilichohitajika.

Kufuatia maelezo hayo,Waziri huyo wa Maji na Umwagiliaji Mh Prof Makame Mbarawa, amemuagiza mkuu wa mkoa wa Mara kuanza kufanya uchunguzi wa kina kuhusu utekelezaji wa mradi huo,huku Mkuu wa mkoa wa Mara Bw Adam Malima,akipokea maelekezo hayo kwa kuagiza taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini kuanza mara moja uchunguzi wa mradi huo mkubwa wa maji.