Back to top

Wakulima Handeni waomba kupatiwa mikopo.

22 July 2018
Share

Baada ya kuhamasika katika kilimo cha mazao ya Muhogo na Korosho wakulima  wilayani  Handeni mkoani Tanga wameiomba serikali kuwapatia mikopo pamoja na zana bora za kilimo ili waweze kulima kilimo cha kisasa.

Hayo yamesemwa na wakulima hao wakati Kamera ya ITV ilipofika kwenye mashamba yao na kuona wakulima hao wanavyojipanga kupokea fursa ya viwanda vya mazao yao vinavyojengwa hapa Handeni.

Kufuatia changamoto hizo mkuu wa wilaya ya Handeni ameziagiza idara za kilimo za halmashauri zote mbili wilayani hapa kuanzisha vitalu vitakavyosaidia wakulima kupata Mbegu kwa urahisi.

Katika hatua nyingine mkuu huyo akatoa maagizo kwa maafisa hao kuwatembelea wakulima waliopewa mbegu bure hasa za mikorosho kuhakikisha mashamba yao yanakuwa safi muda wote