Back to top

Wakulima Simanjiro walia na pembejeo za kilimo

19 June 2018
Share

Wakulima wadogo wa mazao ya chakula kutoka vijiji vya wilaya ya Simanjiro ambao wameamua kupunguza sehemu ya mifugo na kufanya kilimo wamesema ukosefu wa maduka ya kutosha ya pembejeo za kilimo unachangia kurudisha nyuma juhudi za kujikwamua kiuchumi kupitia kilimo.
 
Kauli ya wakulima wameitoa katika maadhimisho ya siku ya wakulima katika wilaya ya Simanjiro wanasema jamii ya kifugaji haikuwa inapenda kilimo baada ya ushawishi kutoka kwa wadau wa maendeleo wameamua kulima lakini changamoto za ukosefu wa pembejeo inawakatisha tamaa ya kuendelea na kilimo wameomba serikali iwasaidie kutatua kero hiyo.

Wadau wa kilimo wanasema mbali na changamoto za ukosefu wa pembejeo pia eneo ilo ni njanda kame ili wakulima wafanikiwe wanapaswa kuzingatia  kilimo  hifadhi chenye kutunza rutuba kwenye udongo usiyo na maji ya kutosha.

Akizingumza na wakulima wakiwa kwenye baadhi ya mashamba ya wakulima Mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mhandisi Zephania Chaula anasema serikali imeshaanza kutatua baadhi ya changamoto kwa kuongeza maafisa ugani na kuwaunganisha wakulima na taasisi za fedha ili wapate mikopo nafuu.