Back to top

Wakulima wa Pamba Kishapu walalamikia kutolipwa fedha za Pamba.

19 February 2020
Share

Wakulima wa zao la Pamba wilayani Kishapu wamelalamikia kutolipwa fedha za Pamba waliyouza tangu msimu wa kilimo uliopita hali ambayo wameitaja kuwa imesababisha washindwe kumudu kutunza familia zao na pia kushindwa kuendelea na shughuli za kilimo katika msimu huu. 


Wakizungumza kwa niaba ya wananchi wa wilaya ya Kishapu wawakilishi wao ambao ni madiwani wamezungumzia shida wanazokumbana nazo wakulima ikiwemo kushindwa kumudu familia zao kwa kununua chakula.

Afisa kilimo na biashara wa wilaya Kishapu George Kessy amezungumzia mfumo wa ununuzi wa pamba katika msimu uliopita akidai kuwa kuna baadhi ya AMCOS zimeshafikishwa mahakamani kwa kutafuna fedha za wakulima.