Back to top

Wakulima wa ufuta Tunduru waomba mizani kukaguliwa mara kwa mara

16 June 2019
Share

Baadhi ya wakulima wa zao la ufuta katika halmashauri  ya wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, wameiomba serikali kupitia wakala wa vipimo mkoani humo kuhakikisha wanakagua mizani kwenye vituo vyao vya kununulia zao hilo mara kwa mara ili kuwabaini makarani wanaochezea mizani makusudi kwa lengo la kuwaibia wakulima.
 
Wakulima hao wametoa ombi hilo wakati wa zoezi la kushtukiza la kukagua mizani inayotumika kupima ufuta wa wakulima kwenye maeneo maghala yanayotumika kukusanya ufuta wa wakulima kwa ajili ya kuuzwa kwa mnada katika wilaya ya Tunduru, zoezi ambalo limefanywa na wakala wa vipimo mkoa wa Ruvuma.

Meneja wa wakala wa vipimo mkoa wa Ruvuma, Bw. Hassan Haletu amesema zoezi hilo la kukagua mizani litakua endelevu na kwamba makarani wote watakaobainika kuichezea watachukuliwa hatua za kisheria.