Back to top

Walala watatu kitanda kimoja kutokana na uhaba wa mabweni

22 April 2019
Share

Wanafunzi wa shule ya bweni ya wasichana ya sekondari Mlongwema iliyopo tarafa ya Mlalo wilayani Lushoto wamekumbwa na hofu ya mabweni yao kuchomwa moto na baadhi ya watu hasa nyakati za usiku kufuatia shule hiyo kukosa uzio ambao ungeweza kuwaweka katika hali ya usalama.

Wakizungumza mbele ya mkuu wa wilaya ya Lushoto pamoja na viongozi wa idara ya elimu wilaya walipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuwahamasisha wanafunzi hao kufanya vyema katika mitihani yao ya kumaliza kidato cha sita inayotarajiwa kufanyika mei 6 mwaka huu ili waweze kupata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu wanafunzi hao wamesema mbali na changamoto hiyo pia katika mabweni wanalala watatu katika kila kitanda hatua ambayo inaweza kuhatarisha afya zao.