Back to top

Walimu Nyasa waaswa kufundisha kwa weledi kuongeza ufaulu wa wanafunzi

21 August 2018
Share

Kutokana na wilaya ya Nyasa mkoa wa Ruvuma kufanya vibaya katika ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, mjumbe wa kamati kuu ya utendaji ya chama cha walimu Tanzania (CWT), Bi. Sabina Lipukila, amewataka walimu wilayani humo kujipima upya na kufundisha wanafunzi kwa weledi mkubwa ili waweze kuleta matokeo chanya zaidi katika ufaulu wa wanafunzi.
 

Akizungumza na walimu wa shule mbalimbali za msingi na sekondari katika wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, mjumbe huyo wa kamati kuu ya utendaji ya chama cha walimu Tanzania (CWT), Bi. Sabina Lipukila amesema hatima ya maisha bora ya watanzania ipo mikononi mwa walimu na kwamba wanapaswa kubadilika na kufundisha kwa weledi mkubwa ili kuongeza zaidi ufualu wa wanafunzi tofauti na hali ilivyo sasa.
 
Hata hivyo baadhi ya walimu wa wilaya hiyo wamesema pamoja na wengi wao kufundisha wanafunzi katika mazingira magumu, kulipwa mishahara kiduchu, kutolipwa fedha za uhamisho pamoja na kutopandishwa madaraja yao kwa wakati kunawavunja moyo wa kazi huku wakiiomba serikali kuondoa ukiritimba huo.