Back to top

Waliochana mabango ya wagombea wa vyama vya siasa watiwa nguvuni.

09 October 2020
Share

Watu 12 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za makosa ya jinai wakiwemo waliochana mabango ya wagombea wa nafasi za ubunge na udiwani wa chama cha CHADEMA na CCM katika wilaya ya Nyamagana na watuhumiwa wa utapeli wa fedha za kigeni . 
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Muliro Jumanne Muliro  amesema jeshi hilo linawashikilia watu wanne akiwemo raia moja wa Uganda ambao wanadaiwa kukiri kujihusisha na matukio ya utapeli wa fedha za kigeni katika mikoa mbalimbali nchini na nje ya nchi.