Back to top

Walionunua Korosho kwa njia ya Kangomba kutolipwa.

10 January 2019
Share

Waziri wa kilimo,Mhe.Japhet Hasunga, amesema wale wote ambao wamenunua Korosho kwa njia ya Kangomba hawatalipwa fedha zao pamoja na Korosho zao licha kuwepo kwenye maghala.

Waziri wa kilimo ameyasema hayo wakati akizungumza  na wajumbe walioshiriki katika kikao  cha kamati ya ushauri mkoa huku akiwashauri wakulima wa Korosho kuendelea kulima zaidi na wasikate tamaa  na changamoto zilizojitokeza.

Kwa upande wao mbunge wa jimbo la Liwale pamoja na mbunge wa kilwa wameiomba serikali kuharakisha malipo ya wakulima kwani wakulima wanashindwa kuwapeleka shule watoto wao kwa kukosa fedha ya kununulia vifaa vya shule.