Back to top

Wanafunzi Kenya wafariki kwa kukanyagana.

03 February 2020
Share

Wanafunzi 13 wa shule ya msingi ya Kakamega nchini Kenya wamefariki dunia na wengine 39 kujeruhiwa baada ya kukanyagana kwenye ngazi ya kushukia kutoka darasani,baada ya kengele ya kumaliza masomo  kugongwa.

Kamanda wa polisi Ukanda wa Magharibi mwa Kenya Peris Kimani  amesema tukio hilo  limetokea wanafunzi walipokuwa wakielekea nyumbani baada ya kukamilika kwa vipindi  jioni ya leo.

Kamanda Kimani amethibitisha kuwa wanafunzi 20 wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani.