Back to top

Wanafunzi Mtwara, Lindi waomba maziwa ya korosho yawe mbadala wa uji.

05 August 2020
Share

Wanafunzi wa shule za msingi katika mikoa ya Lindi na Mtwara wametaka maziwa ya korosho kunywewa mashuleni badala ya uji huku watafiti wa zao la korosho kutoka TARI Naliendele wakisema zao hilo linakinga kubwa katika mwili wa binadamu hasa kwa kundi la watoto na wazee.

Kauli hiyo ya watoto imekuja ikiwa Bodi ya Korosho na Kituo cha Utafiti wa Kilimo (TARI) Naliendele wakijiandaa kuadhimisha siku ya kula na kunywa  korosho itakayofanyika Agosti 06 katika viwanja vya Nanenane Ngongo mkoani Lindi.