Back to top

Wanafunzi shule ya sekondari Mlowa wajengewa Bweni na TASAF

20 August 2018
Share

Wanafunzi wa shule ya sekondari Mlowa mjini Makambako mkoani Njombe wanaofikia zaidi ya 300 wameishukuru serikali kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF awamu ya tatu kwa kukamilisha ujenzi wa bweni moja la wasichana litakalochukua wanafunzi zaidi ya 900 kwa kugharimu milioni 64.

Wakizungumza na ITV wanafunzi shuleni hapo wamesema kuwa wanatarajia kupandisha ufaulu Katika masomo yao baada ya kuhamia katika bweni hilo kwa kuwa kwa sasa baadhi yao wanaishi madarasani na wengine wakitembea umbali mrefu kutoka nyumbani na kushindwa kuzingatia masomo.

Makamu mkuu wa shule ya Sekondari Mlowa Peter Chura tula amesema kuwa watoto wakiwa katika bweni wataepukana na vishawishi vinavyopelekea kupata ujauzito huku akiomba tasafu kusaidi bweni ujenzi wa bweni la wavulana.

Afisa ufuatiliaji wa TASAF makao makuu katika halmashauri za mji makambako ,wangingo'mbe na mbarali Edwin Mlowe amesema kuwa TASAF itaendelea kushirikina na wananchi katika kupunguza changamoto hasa katika sekta ya elimu.