Back to top

Wanafunzi walikosa nafasi kidato cha kwanza, kuanza masomo Machi.

16 February 2019
Share

Serikali imewataka wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, miji, manispaa na majiji kuhakikisha wanakamilisha haraka iwezekanavyo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za sekondari za kata ili kuruhusu wanafunzi waliokosa nafasi za kuingia kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa, wanaanza masomo yao mapema mwezi Machi.

Katibu Mkuu Ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa ( TAMISEMI ) Mhandisi Joseph Nyamhanga ametoa maelekezo hayo wilayani Nyamagana mkoani Mwanza wakati akikagua ukarabati wa vyumba vya madarasa, vyoo na jengo la utawala katika shule za sekondari Nyegezi na Fumagila, pamoja na ujenzi wa majengo 6 katika kituo cha afya Igoma jijini Mwanza, miundombinu ambayo imegharimu zaidi ya shilingi milioni 600.