Back to top

Wanajeshi wastaafu walalamikia kutopata tiba bure.

15 June 2019
Share

Wanajeshi wastaafu nchini ambao wengi wao wamepata ulemavu wa kudumu wakati wa vita baina ya Tanzania na Uganda iliyoanza mwishoni mwa mwaka 1978,wameiomba serikali kuwaingiza katika utaratibu wa kupata matibabu bure kama ilivyo kada nyingine za serikali kutokana na changamoto kubwa za kiafya zinazowakabili .

Wakizungumza jijini Tanga mbele ya wanajeshi wastaafu,viongozi ngazi ya mkoa na taifa  wa muungano wa wanajeshi wastaafu nchini,wamesema wanajeshi wanapostaafu hawaruhisiwi kupata matibabu bure kama ilivyo kada nyingine za serikali hatua ambayo imewaathiri kiafya ingawa wametoa mchango mkubwa kwa taifa hili.

Mwenyekiti wa muungano huo kitaifa Bwana Assed Mayuki amesema wameanza mchakato muda mrefu wa kuomba ridhaa kwa viongozi ngazi ya taifa ya kupata matibabu bure na badala yake hadi sasa zoezi hilo bado kufanyiwa kazi.

Kufuatia hatua hiyo baadhi ya wanajeshi waliopata ulemavu wa kudumu koplo mwibale humbu amesema hadi sasa na ulemavu aliokuwa nao baada ya kulipukiwa na bomu katika vita amesema amehangaikia stahiki zake lakini hadi sasa hajui atapata wapi msaada ili kufanikisha zoezi hilo.