Back to top

Wananchi Geita wafyeka kujenga Zahanati.

27 May 2020
Share

Wakazi wa kata ya Bombambili mkoani Geita wamejitolea kufyeka pori ili kujenga zahanati katika eneo hilo kuondoa adha ya wakinamama wajawazito kusafiri umbali mrefu kufuata huduma za afya.

ITV ilifika katika eneo  la Bombambili na kushuhudia wananchi hao wakiendelea na uchimbaji msingi na ufyekaji pori huku wakiiomba serkali kuwaunga mkono katika ujenzi huo.

Akizungumza katika zoezi hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Geita  mhandisi  Modest Apolinari amesema atatoa tofali zaidi ya elfu ishirini na  saruji ili kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo.

Naye Mkuu wa mkoa wa Geita mhandisi Robert Gabriel amesema wameweka mpango maalumu wa kuwaunga mkono wananchi wanaoanzisha ujenzi wa zahanati kila kijiji ili kuhakikisha majengo yote yanakamilika kwa wakati ili wananchi waondokane na adha ya upatikanaji wa huduma ya afya.