Back to top

Wananchi Madaba Songea waonyesha jitihada kutatua tatizo la maji.

10 July 2018
Share

Wananchi wa  kijiji cha  Lilondo halmashauri ya wilaya ya Madaba wilayani Songea mkoani Ruvuma wamejitokeza kwa wingi kuchimba  Mitaro na kufukia mabomba katika mradi wa maji wa Lilondo  utakaogharimu shilingi milioni 6o hadi kukamilika ili kutatua  tatizo la maji katika kijiji chao.

Wananchi hao wanasema kuwa wameamua kuchukua hatua  badala ya kuisubiri serikali kwa kila kitu  na  kuona katika kijiji chao kuna shida kubwa ya maji  ambapo hadi sasa wametumia shilingi milioni 20 katika mradi huo.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Madaba Mheshimiwa Joseph Mhagama amechangia  shilingi milioni tano na mabomba ili kutatua tatizo la maji katika kijiji cha Lilondo.

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Madaba Bw. Vastus Mfikwa amemshukuru mbunge Joseph Mhagama kwa kushiriki katika kuchimba mtaro na kutandaza  mabomba katika mradi huo.